Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mazungumzo ya Iran na Saudia yalianza katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad miezi kadhaa iliyopita na pande mbili hadi sasa zimefanya duru tano za mazungumzo ikiwemo ile iliyofanyika hivi karibuni mjini Baghdad.
Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimi amesema Iran na Saudia zimepiga hatua kubwa katika mazungumzo na amebainisha matumaini yake kuwa pande mbili zitafikia mapatano hivi karibuni.
Al -Kadhimi amesema eneo haliwezi kupata ustawi na maendeleo ya kiuchumi bila kutatuliwa matatizo na migogoro baina ya nchi.
Ameongeza kuwa sera za kigeni za Iraq zimejengeka katika msingi wa uhusiano wenye mlingano na nchi zote huku akisisitiza kuwa nchi yake si tishio kwa majirani.
342/